Where are you from? | Unatoka wapi? |
I am coming from the city of New York | Ninatoka jiji la New York. |
Where are you staying now? | Unakaa wapi sasa? |
I am staying in a student hostel | Ninakaa katika bweni. |
In which street? | Katika Njia gani? |
In which neighborhood? | Katika mtaa gani? |
Where are you studying now? | Unasoma wapi sasa? |
I am studying at the University of California Los Angeles. | Ninasoma katika Chuo Kikuu cha California Los Angeles. |
What are you studying? | Masomo gani unasoma? |
I am studying Swahili and linguistics. | Ninasoma Kiswahili na isimu ya lugha. |
Is Bill studying Swahili now? | Je, Bill anasoma Kiswahili sasa? |
Who is teaching Swahili? | Nani anafundisha Kiswahili? |
Why are you studying Swahili? | Kwa nini unasoma Kiswahili? |
I want to travel to Tanzania in order to make research. | Nataka kuenda Tanzania ili kufanya utafiti. |
Which language is he studying? | Anasoma lugha gani? |
Where are the teachers coming from? | Walimu wanatoka wapi? |
What are you teaching? | Unafundisha nini? |
Who is coming from New York? | Nani anakuja kutoka New York? |
Sarah is a Swahili teacher. | Sarah ni mwalimu wa Kiswahili. |
She’s from Mombasa but she’s staying in the city of Los Angeles now. | Anatoka Mombasa lakini anakaa katika mji wa Los Angeles sasa. |
She’s teaching Swahili here in America and studying linguistics at the University. | Anafundisha Kiswahili hapa Amerika na anasoma isimu katika Chuo Kikuu. |
After getting her degree she wants to return to Kenya and to teach linguistics at the University of Nairobi. | Baada ya kupata digrii yake anataka kurudi Kenya na kufundisha isimu katika Chuo Kikuu cha Nairobi. |
Teacher Tom is a teacher of linguistics and he’s teaching Swahili, as well. | Mwalimu Tom ni mwalimu wa isimu na anafundisha Kiswahili, pia. |
His wife is coming from the city of Michigan. | Mke wake anatoka mji wa Michigan. |
Her husband and their children are staying in Los Angeles. | Mume wake na watoto wao wanakaa Los Angeles. |
He’s working in the laboratory of UCLA. | Anafanya kazi katika maabara ya UCLA. |
Who is coming from Mombasa? | Nani anatoka Mombasa? |
Which language is Mrs. Sara teaching? | Bibi Sara anafundisha lugha gani? |
Where is teacher Tom‘s wife working? | Mke wa mwalimu Tom anafanya kazi wapi? |
What is the teacher’s name? | Jina la mwalimu ni nani? |
Do you live in Dar es Salaam? | Je, unaishi Dar es Salaam? |
We want to study Swahili. | Tunataka kusoma Kiswahili. |
We are coming from Mombasa. | Tunatoka Mombasa. |
Where are you guys coming from? | Ninyi mnatoka wapi? |
They are studying Swahili. | Wanasoma Kiswahili. |
The old men are greeting each other. | Wazee wanaamkiana. |
I want to study Swahili. | Nataka kusoma kiswahili. |
The old men are teaching. | Wazee wanafundisha. |
I want to get a Swahili course. | Nataka kupata kozi ya Kiswahili. |
African studies | Masomo ya Kiafrika |
architecture | usanifu majengo |
business | biashara |
chemistry | kemia |
communication studies | masomo ya mawasiliano |
developmental studies | masomo ya maendeleo |
economics | uchumi |
education | elimu |
engineering | uhandisi |
environmental science | sayansi ya mazingira |
finance | elimu ya fedha |
fine arts | sanaa |
geography | jiografia |
geology | jiolojia |
history | historia |
law | sheria |
library science | sayansi ya maktaba |
literature | fasihi |
management | uongozi / manejementi |
Mathematics | hisabati / hesabu |
medicine | udaktari / uganga |
meteorology | meteorolojia |
music | muziki |
nutrition | lishe |
pediatrics | matiababu ya watoto |
philosophy | falsafa |
physics | fizikia |
plant science | sayansi ya mimea |
political science | sayansi ya siasa |
religion | dini |
science | sayansi |
social science | sayansi ya jamii |
surgery | upasuaji |
theatre arts | sanaa ya maonyesho |
urban planning | mipango miji |
women's studies | Masomo ya wanawake |